Stadi za Maisha ni ujuzi ambao sio rahisi
watoto au vijana wapate katika mitaala ya kawaida darasani au vyuoni. Familia za
kibiashara na kijasiriamali
zimekuwa zikiwafundisha ujuzi huu watoto wao na hivyo kuwa na duara la
mafanikio katikati yao tu huku familia nyingi za kisomi zikiwasisitizia
watoto wao elimu tu kama ndio njia kuu ya kufanikiwa kimaisha.
Funguka, kama unamtakia mtoto/kijana wako maisha bora ya baadaye mfundishe au muelekeze stadi za maisha zifuatazo:
- Namna ya kuandaa bajeti ya pale nyumbani kwako
- Kulipa bili mbali mbali kama za startimes, tanesco, maji nk
- Kufanya manunuzi sokoni na supermarket
- kufix matatizo madogomadogo pale nyumbani kama ya umeme, maji, TV, vitasa vya nyumba, rangi, nk
- Nenda naye kazini kwako hasa wakati wa likizo na kumfundisha kazi
zako taratibu kama fursa inaruhusu mfano namna ya kupiga simu za
kiofisi, naman ya kuandika na kutuma email, naman ya kutuma na kupokea
faksi, naman ya kuprint na kutoa photocopy, namna ya kuscan, namna ya
kuafail na kutoa baryua kwenye mafail (badala ya kumpeleka tuition)
- Mzoeshe utoaji mfano kanisani mpe sadaka akatoe yeye kwa niaba yako
au mpe sadaka kama yako. wewe ukitoa 5,000 na yeye mpe elfu tano kama
huna basi wewe baki mpe mtoto akatoe kwa niaba yako. Mzoeshe pia kutoa
kwa maskini na wenye uhitaji
- Mzoeshe kuwaombea wadogo zake, wakubwa zake, majirani, marafiki na maadui
- Mfundishe na umzoeshe kufanya biashara ndogo ndogo (kulingana na umri wake)
- Mzoeshe kuongoza ibada ya nyumbani na kufanya maombi
- Mzoeshe kwenda kusalimia marafiki na majirani wa karibu (close friends and relatives)
- Mzoeshe kusema samahani anapokosea na asante anapofanyiwa wema na kusema nimekusamehe anapoombwa samahani
- Mzoeshe kusifiwa mwenzake hasa wadogo zake au wakubwa zake pale wanapofanya vizuri hata kama ni kwa haba
- Mzoeshe kuwa mdadisi wa mambo (critical thinker) Mfano kwani ukirusha kitu juu inarudi chini, kwa nini, kwa nini? nk
- Mzoeshe kuuliza kwa nini kwa kila jambo analofanya (mfano kwa nini anasoma, kwa nini anatakiwa kufanya usafi wa kinywa nk)
- Mzoeshe mtoto kusoma (mfano vitabu, magazeti, majarida yenye kuelimisha)
- Mzoeshe mtoto kutambua vipawa na vitu anavyovipenda kufanya ili aviendeleze
- Mzoeshe mtoto kupenda wenzake kwa matendo.( mfano kumwomba Mungu
amuwezeshe kupenda wengine, kuwaombea wengine wapate mafanikio kwa
Mungu, kuwapa zawadi wadogo zake na wakubwa zake -akinuanua pipi mbili,
moja yake na moja ya rafiki yake au mdogo wake au mkubwa wake)
- Jizoeshe kutoka out kama za lunch na mtoto wako
- Jizoeshe kupumzika na mtot0 wako na kufanya yale mambo mtoto
anafanya (mfano kuangalia TV pamoja,, kuangalia mechi za mpira pamoja,
kwenda kutembea pamoja ili uweze kumjua mtoto wako na anapendelea mambo
gani na pia upate fursa ya kumuelekeza kwenye mambo yanayofaa zaidi)
- Fanya matukio kama ya birthday pamoja na mtoto wako huku akiwaalika
marafiki zake wa karibu (hii itakuwa fursa yako ya kuwafahamu marafiki
wa mtoto wako)
- Mzoeshe mtoto ajifunze kuwasikiliza wengine kwanza sio yeye tu asikilizwe
- Unapombeba mtoto wako kwenye gari muelekeze mambo kadha wa kadha mfano kuwasha gari, kuzima, kushika mbreki, kutumia usukani nk)
- Mzoeshe mtoto kuweka kumbukumbu kwa kuandika na jinsi ya kufail kw
ampangilio, mfano matokeo yake yawe kwenye faili la kwake ambalo yeye
mwenye analisimamia
- Mzoeshe mtoto namna ya kutengeneza ratiba na kuifuata mfano ratiba
ya siku, kuamaka, kufanya usafi, kwenda shule, kujisomea, kufanya
homework, kufanya kazi za nyumbani, kucheza kuangalia vipindi maalum za
TV au kanda nk
- Mtoto ajizoeshe kuandika maono na malengo ya maisha yake ya muda mfupi, kati na mrefu
- Mzoeshe mtoto kutumia usafiri wa umma kama daladala
- Mzoeshe mtoto kuwasiliana naye kwa barua ili azoee kuandika barua
nzuri mfano za maombi ya vitu vinavyotakiwa shuleni na bei yake
- Mzoeshe pia mtoto kufanya window shopping kwa vitu vya shuleni na zile za nyumbani kama vyakula na vifaa vingine vya nyumbani
- Mzoeshe mtoto kutumia kompyuta kwa matumizi madogomadogo kama ya kuanda bajeti kwa excel na kuandika maombi kwa MS Word
- Mzoeshe mtoto kuogelea hasa kwa wale walio karibu na mito, maziwa na bahari
- Mnunulie mtoto kamera ndogo ya kujifunzia na awe anatumia kwenye matukio muhimu makanisani, shuleni nk
Hakuna maoni: