ELIMIKA NA : Chris Mauki..........Hatua Kumi Za Kukuwezesha Kupanda Daraja Katika Maisha
Posted by Unknown ~ on
Jumamosi, 14 Desemba 2013 ~
Watu wengi hutamani sana kupandishwa vyeo baada ya kuchoka sana
na nafasi walizokuwa nazo kwa muda mrefu, au pia wengine wanatamani sana
kupandishwa vyeo kwasababu ya kuongeza kipato ili kufikia malengo
fulani maishani, kilammoja ana sababu binafsi ya kuhitaji kupandishwa
cheo. Taarifa za kupandishwa cheo ni za kufurahisha kwa kila mmoja wetu,
wako ambao kuilazimisha fursa hii hata kwa kwenda kwa waganga, kuhonga,
kujipendekeza, kujitoa miili yao na njia nyingine nyingi ili tu kupata
cheo. Mara nyingi tumejiuliza kwanini sipandi cheo, wengine wapya
wanakuja hapa wanafanya kazi kidogo mara wanapandishwa cheo,
wanabadilishiwa ofisi, wanapata gari la ofisi, nyumba, na marupurupu
mengine lakini sio mimi, ukweli ni kwamba sababu kubwa ni sisi wenyewe,
vitu vinavyotuangusha na kutufelisha sio vile vilivyo nje yetu bali vile
vilivyo ndani yetu, yaani vilivyo ndani ya uwezo wetu. Leo unaweza
kuamua kufanya jitihada binafsi za jujua namna ya kuweza kupandishwa
cheo. Yamkini wewe ni mmoja wa hawa ninaowazungumzia hapa ili uweze
kujikwamua
Jaribu kufuata kanuni hizi rahisi:
1. Jitahidi kujuana na watu.
Unaweza
kufikiri kuwa njia pekee ya kubadilisha mazingira uliyonayo ni kukaa na
kuwaza sana, hapana, hii siyo kweli, jaribu kujipenyeza kufahamiana na
wengine, usijitenge sana, shiriki maisha yako na wale walioko karibu
nawe.
Usifikiri kuwa wewe hustahili kujichanganya katika mazungumzo
ya kawaida na watu wa ofisini kwako, usifikiri kuongea na bosi wako
masuala ya kawaida ni kujipendekeza, kumbuka kwa kuwajua na
kujichanganya na wafanyakazi wenzako tunajenga nguvu ya umoja wa kazi,
taratibu wote tunakuwa ni timu moja katika utendaji.
2. Usijifanye mkamilifi katika kilakitu.
Pia
usibaki umefungiwa katika kiti chako au meza yako ya kazi hata zile
nyakati ambazo wengine wanapumzika au kujiburudisha, kama kuna hafla ya
ofisi na wenzako wanaenda basi shiriki nao, usifikiri wanapoteza muda,
kama mwenzako anatukio fulani la furaha nyumbani basi usiche kushiriki,
na kama wewe unatukio kama hilo kwako basi wakaribishe wenzako na
usisahau kumualika hata na bosi wako pia. Taratibu unapoanza kumfahamu
zaidi bosi wako ni mwelekeo mzuri katika kuelekea mafanikio yako.
Usije
ukafikiri kuwa haukuumbiwa kufanya makosa, kufanya kosa kupo katika
maisha ya mwanadamu. Kama wewe nimtu unayefanya kazi sana sio kitu cha
kushangaza sana ukikosea kitu. Ikiwa unatokea kufanya kosa, basi usikae
ukijilaumu nakujiuliza kwanini umefanya kosa bali jifunze, pata somo
katika kukosea kule na uendelee mbele. Kama utaweka akili yako yote
katika kujichunguza kila kitu unachokifanya iliusikosee basi hata basi
wako anaweza kufikiri kuwa wewe nikati ya wanaojifanya wakamilifu katika
kila wafanyalo na kinyume chake cheo kikaenda kwa wenzako na sio wewe.
Usisahau kuwa waweza kujikuta unafanya vimakosa vingi zaidi wakati
unajitahidi kujiweka mkamilifu katika jambo.
3. Kuwa mwaminifu.
Uaminifu
ni kitu kizuri na cha maana sana na kinachowashinda wengi wetu. Wakati
wowote unapopata nafaasi ya kuongea na bosi wako, kuwa mkweli katika
kila neno litokalo kinywani mwako, liwe dogo au kubwa, liwe kuhusu wewe
mwenyewe au kuhusu mtu mwingine, kuwa mkweli hata katika yale
yanayoonekana kukuathiri wewe, amua kuwa mkweli bila kujali mazingira.
Kuwa mkweli katika yale unayoyatamani na katika maswala mazima ya
maendeleo ya kazi yako, sio tu unazungumza kile unachofikiri bosi wako
angetamani ukiseme.Staili za kuongea zaweza kutofautiana mtu na mtu
lakini ujumbe ubaki kuwa wa kweli.
4. Penda mazingira masafi.
Wakati
wowote penda kuyaweka mazingira yako ya kazi safi, hatakama ofisi sio
ya kuvutia sana lakini bado unaweza kuvipanga vitu katika meza yako au
pale unapofanyia kazi vikawa vema na vyenye mpangilio mzuri. Wengine
wamekuwa wakijidanganya kuwa kama wakipoteza muda wao kufanyia usafi
eneolao lakazi basi mabosi wao wataona kuwa hawana kazi za kutosha za
kufanya, hii ni kinyume kwa maana hali yako ya ndani ya kiutendaji
yaweza kuonekana pale tunapotazama mazingira ya wewe unapofanyia kazi.
Maranyingi
wengi wetu tumejidanganya kuwa kwa kufanya kazi masaa mengi sana,
kutoka usiku makazini na kuwahi kufika mapema sana asubuhi ndio
tunaandaa mazingira ya kupanda vyeo, bado kuwaza hivi ni kosa.
Ukiendelea hivi kwa muda wanaokuzunguka pamoja na bosi wako wanapata
ujumbe kuwa unahangaika sana na majukumu yako yanayoonekana kukushinda
na hivyo itakuwia ngumu sana kukabidhi kazi katika wakati muafaka.
5. Fanya kazi katika masaa sahihi.
Kama unadhani
unahitaji kufanya majukumu ya zaidi ili upate changamoto za ziada basi
inakubidi ukubali kujitolea kutoa msaada katika baadhi ya majukumu ya
wengine pale inapobidi. Waweza kuzungumza na bosi wako kuhusu hili pia,
jitahidi kuwa halisi zaidi katika matazamio yako na usiweke malengo
yaliyo juu ya uwezo wako ka unajua hutoweza kuyatimiza.
6. Jitahidi kufanya majukumu ya zaidi.
7. Uliza maswali.
Kukaa
kimya tu huku umeinamisha kichwa chini pasipo kusema kitu
hakutakusaidia chochote katika kupanda cheo, Usihofu kuuliza swali
lolote na kama unakitu au wazo juu ya jinsi gani halifulani inaweza
kuboreshwa basi iseme kwa wahusika. Yawezekana ukajiona kama
unayepitiliza mipaka yako ya kazi, na yamkini wengine wasikuelewe,
lakini usihofu maana taratibu itawaonyesha kuwa unaipenda kazi na uko
tayari katika kuboresha biashara au mafanikio ya ofisi kwa ujumla.
8. Fanya utafiti.
Kama
unakiu ya kupanda ngazi katika masuala ya kikazi na ajira basi lazima
ufanye tafiti, kama kuna kazi maalumu unataka kuiomba hakikisha unajua
kilakitu kuhusu kazi hiyo na uweze kuelezea jinsi gani ujuzi wako
unaendana na ule unaohitajika katika kazi husika.
9. Jifunze kutengeneza nafasi mpya
Kama
unafikiri kuna njia rahisi zaidi au za mafanikio zaidi katika utendaji
wako wa kazi au kama unaona umuhimu wa kuwepo kwa nafasi nyingine ya
kazi ni bora uzungumze na bosi wako. Kwa sababu wewe ndiyo uliyeona
umuhimu wa nafasi hiyo na kulitolea wazo, kuna uwezekano mkubwa kwamba
wewe ndiyo utakayeonekana kufaa kuchukua nafasi hiyo, hii inamaanisha
kwamba utakuwa tayari kubeba majukumu mapya.
10. Ongeza ujuzi wako.
Kama unaona
kunaumuhimu wa kuongezea kidogo ujuzi ulionao basi tafuta kozi
zinazoendana na kile unachotaka kukifanya, jitahidi kuhudhuria semina,
warsha na makongamano mbalimbali ya mlengo wa kazi yako, penda kujua
zaidi ya vile wenzako wanavyovijua. Waweza kuwauliza waajiri wako kama
kuna fungu kwa ajili ya kujiendeleza ili ulifaidi, onyesha kuwa unakiu
ya kujiongezea ujuzi kwa manufaa ya kampuni au ofisi, hii itawafurahisha
wakuu wako na kupanua wigo wa kukufikiria kwa majukumu makubwa zaidi.
Onyesha
mafanikio yako kwaundani iwezekanavyo lakini pasipo kujikweza au
kujisifia, mfano; kama umefanikiwa kuvuka malengo ya mauzo yako kwa
kipindi fulani, basi acha mabosi wako walijue hilo.Mara uchukuapo jukumu
fulani ilikulifanya basi jitahidi kuonyesha kuwa unalifurahia na wala
haulijutii, fanya kila ulilosema kuwa utalifanya, na kwa hivyo
utaonyesha heshima kubwa na kujionyesha mtu unayeweza kutegemewa. Ni
muhimu sana kuwa na tabia hizi kwa maendeleo binafsi.
Na: Chris Mauki
University of Pretoria
South Africa
chriss@udsm.ac.tz
Related Posts
Hakuna maoni: