Kilimo cha kutumia mahema chainua uzalishaji wa kilimo nchini Kenya
Posted by Unknown ~ on
Jumamosi, 14 Desemba 2013 ~
Wakikabiliwa na eneo dogo la kulima kutokana na kukua kwa idadi ya
watu na hali za hewa zisizotabirika, wakulima wengi wa Kenya wamegeukia
teknolojia ya kilimo cha mahema kama njia ya kuongeza uzalishaji na
kunyanyua kipato chao.
Kukua kwa umaarufu wa kilimo wa mahema kulioneshwa katika Maonesho ya
Biashara ya Kimataifa ya kila mwaka mjini Nairobi mwezi wa Oktoba
ambapo waoneshaji wa kilimo cha kutumia mahema walisema kuwa waliona
kuinuka kwa hamu ya umma katika kilimo hicho.
"Wakenya wengi wameanza kufuata kilimo cha kutumia mahema kwa sababu
kinahitaji mtaji mdogo ili kuanzisha na wakulima wanaweza kuzalisha
zaidi katika shamba dogo," alisema Moses Khaemba wa Kampuni ya Hortipro
Limited, iliyoko Nairobi ambayo inatengeneza mahema ya kilimo kwa
gharama ndogo.
Pamoja na kuwa inakuwa ya gharama ndogo na rahisi kuyaweka, mahema ya
kilimo pia gharama ndogo ya ushughulikiaji, yantumia maji kwa ufanisi
na yanaweza kuhamishwa baina ya vitalu, alisema, na kuongeza kuwa
wakulima wanaweza kuona faida yake kuanzia mavuno ya kwanza.
"Kilimo cha kutumia mahema ya plastiki kina faida nyingi," Khaemba
aliiambia Sabahi. "Faida hizi ni pamoja na uzalishaji wa juu zaidi na wa
kuendelea kwa kila ekari moja, jambo lenye maana ya kupata faida kubwa
zaidi, kujikinga na masuala ya hali ya hewa kama vile ukungu na upepo,
kutokuwepo na hatari ya wadudu waharibifu, kupata mwanga asilia na
upitishaji wa hewa, miongo mirefu ya upandaji na matumizi madogo ya
maji, hasa katika maeneo yenye ukame."
Ukubwa wa mahema ya kilimo unategemea na uwezo wa mkulima wa
kuyashughulikia na ukubwa wa shamba, alisema. Wastani wa kila hema moja
ni upana wa mita 8 na urefu wa mita 30 na hugharimu shilingi 150,000
(dola 1,800). Kampuni imepokea zaidi ya maombi 1,000 ya mahitaji kutoka
kwa wakulima mwaka huu -- ongezeko la asilimia 25 ikilinganishwa na 2011
-- vivyo hivyo na ongezeko la mahema mengi katika shamba hilo hilo,
Khaemba alisema.
Mahema ya kulimia yanaweza kuwa ama katika muundo wa jadi kama nyumba
au muundo wa upenyo - marefu yakiwa yamefunikwa kwa plastiki juu ya
mazao. Wakulima wasema kwa kutumia mahema yenye umbo la upenyo, wanaweza
kuzalisha zaidi kuliko katika ardhi ya wazi.
"Mimi ninayo mahema mawili katika shamba langu la ekari tatu huko
Karen Estate mjini Nairobi ambako nimepanda nyanya," Margaret Wanjiku,
mweny umri wa miaka 54, aliiambia Sabahi.
Wanjiku, ambaye alistaafu miaka mitano iliyopita kutoka shirika moja
la kimataifa la msaada, alisema kuwa mmea wa nyanya unaweza kuzalisha
kilo 16 hadi 20 za nyanya.
Ingawa bei hubadilikabadilika kutokana na upatikanaji wa bidhaa na
mahitaji, alisema kuwa kila mita mraba moja ya nyanya humuingizia kiasi
cha shilingi 3,000 (dola 35). "Ninauza nyanya zangu kwenye duka kubwa
iliopo karibu na nyingine kwa majirani zangu," alisema.
Amos Karanja ametenga sehemu ya shamba lake la robo ekari huko
Kitengela, Jimbo la Kajiado, kwa ajili ya kulima nyanya ndani ya mahema.
"Ingawa ninayo kazi ya mchana, ninajaribu aina hii ya kilimo kama njia
ya kupata mapato ya ziada ili kuisadia familia yangu," aliiambia Sabahi.
Dan Wanjohi kutoka kampuni Daner Greenhouse Limited huko Ongata
Rongai, eneo la makazi ya watu katika Mkoa wa Bonde la Ufa, alisema kuwa
kimwonekano aina yoyote ya mboga inaweza kulimwa katika mahema ya
kilimo, ikiwa ni pamoja na matango, vitunguu na kabichi.
"Wakulima wengi nchini Kenya wanapendelea kulima nyanya kwa sababu ni
mmea unaotoa mazao mengi na mtu hupata faida ndani ya miezi mitatu
baada ya kuotesha," aliiambia Sabahi.
Alisema kuwa kampuni yake inatumia chuma cha pua katika ujenzi wa
hema la ukubwa wa mita 8 kwa 30 na huuzwa kwa shilingi 200,000 (dola
2,300) kwa moja. Gharama ni pamoja na kulaza bomba kwa ajili ya
umwagiliaji maji kwa matone.
Hata hivyo, wakulima ambao hawawezi kumudu gharama za majengo ya
chuma cha pua, bado wanaweza kutumia mahema ya vipenyo kwa kutumia mbao
kwa gharama ya chini zaidi. "Nililipa shilingi 70,000 (dola 818) kwa
kujenga hema langu," Karanja aliiambia Sabahi.
Related Posts
Hakuna maoni: