Kwa sasa ni jina maarufu sana hapa Tanzania, mtu yeyote aliyefanikiwa
katika biashara hupewa jina hili. Maana ya ujasirimali inabaki katika
uwezo wa kufanya maamuzi sahihi wa kutumia rasilimali chache
zinazokuzunguka vizuri ili uweze kupata faida.
Mathalani rasilimali zinazokuzunguka ni ardhi, watu na maji, ni vipi
mchanganyiko huu utautumia vizuri ili uweze kupata zao (output) ambayo
itakusaidia kujikwamua katika hali uliyonayo. Ama ni vipi utatumia mtaji
mdogo ulionao kufanya biashara itakayokuletea faida ambayo utaitumia
kuongeza mtaji na kuikuza biashara yako.
Fahamu kwamba lengo lolote la mjasiriamali ni kupata faida na
kumridhisha mteja ambaye anatumia bidhaa ama huduma inayotolewa na
mjasiriamali. Bidhaa ama huduma ndio msingi wa mjasirimali yeyote ambaye
anataka kupata faida. Mathalani mkulima wa mahindi bidhaa yake ni
mahindi hivyo atauza mahindi kujipatia faida, na mtabibu wa mifugo
anatoa huduma ya matibabu kwa mifugo na kulipwa ujira kwa kutoa huduma
hiyo.
Hakuna maoni: